TIMU ya Magereza Iringa inatarajia kuchuana vikali na timu ya
Mkamba Rangeres ya Kilombero, mkoani Morogoro, katika mechi
itakayofanyika kesho, kwenye uwanja wa Samora.
Akizungumza na blog hii, Katibu wa timu ya Magereza (African
Wonderers fc) ya mjini Iringa, Shukuru Steven alisema wanatarajia kuibuka na
ushindi mnono katika ligi hiyo.
Alisema timu yake imejiandaa vyema kuingia kwenye mpambano
huo, huku wachezaji wote wakiwa na afya njema.
“Hakuna majeruhi hata mmoja na tunatarajia kuibuka washindi
katika mechi hiyo ya kesho tarehe 13,12/2014,” alisema Shukuru.
Shukuru amewataka wananchi wa Iringa kujitokeza kwa wingi
katika uwanja wa Samora ili kuishangilia timu yao.